Monday, 6 June 2016

GODFREY FREEDOMAN’S FUND

High fiveMWENDELEZO WA MPANGO WA KUHAKIKISHA KIJANA ANAJITEGEMEA KATIKA MASWALA YA KIUCHUMI NA MAISHA KWA UJUMLA:

GODFREY FREEDOMAN’S FOUNDATION katika kuhakikisha kuwa kijana anchukuwa nafasi yake ya chachu katika jamii hasa katika maswala ya kiuchimi na maisha kwa ujumla inendeleza harakati zake za kuendelea kuhamasisha vijana ili waendelee kutumia nafasi walizonazo kama fursa ya kujikomboa na umasikini na kuudhihirishia umma kuwa kijana ni chachu ya maendeleo katika Taifa lolote lile. Hivyo basi katika mada iliyopita tuliona ni kwa namna gani kijana anayeishi kijijini anavyoweza kujikomboa na umasikini kwa kutumia mazingira yake bila hata ya kusafiri kwa ajili ya kutafuata maisha. Leo pia tunaendelea na mada yetu hasa kwa vijana waoishi mijini, mara nyingi tumekuwa tikisistizwa kufanya kazi kwa bidii ili tuondokane na umasikini lakini hatujui kuwa kufanya kazi tu haitoshi bali kufanya kazi kwa kujiwekea malengo ndiyo swala muhimu katiaka swala zima la ufanikishaji wa maisha. vijana wengi tumekuwa tukifanya kazi lakini hatuthamini kipato tunachopata kutokana na kazi hiyo kwani  tumekuwa tukidhani kuwa kipato tunachopata ni kidogo sana hivyo basi kinatutosheleza kufanya mahitaji madogomadogo tu jambo ambalo sio la kweli. Sawa kipato chetu ni kidogo na kinatosha mahitaji madogomadogo lakini sas hebu tumia hicho kidogo unachopata ili kutafuta kikubwa ambacho wewe unakihitaji. Mfano tuchukulie   wewe ni kinyozi, kibarua, mpiga debe, bodaboda, daladala (mwendesha baiskeli), muuzaji wa bidhaa ndogondogo yaani karanga, pipi maji n,k. Hapa nataka kuongea hawa watu ni kwanamna gani wanaweza kuwa matajiri kwa kutumia kaipato cha kazi zao bila ya kuwezeshwa na mtu mwingine ila tu kwa kutegemea kipato chao na huku maisha yanendelea. najua wengi mtaniuliza mwendesha baiskeli atawezaje kupata pesa ya kumfanya aache kuendesha baiskeli wakati gharama wanazobebea abiria ni kidogo saana kiasi kwamba pengine hazitoshi kukidhi mahitaji ya siku ktk familia mimi nasema si kweli kwani hakuna mtu anayeweza kufanya kazi ambayo haiwezi kumwezesha hata kupata mlo wa siku moja na kama unaamini hivyo jiulize kama haimwezeshi kupata mlo hata wa siku moja anapata wapi chakula kinachompa nguvu ya kuja kufanya kazi, tena kazi ngumu? Nachotaka nikushauri wewe ambae uko katika hili hizo nilizozitaja hapo juu unachotakiwa kufanya ni kunzingatia yafuatayo:-

  • kwanza kabisa angalia unapta shilingi ngapi baada ya mizunguko yako ya siku.
  • pili angalia matumazi yako muhimu ya siku yanagharimu shilingi ngapi. Napozungumzia mahitaji muhimu nina maanisha mahitaji ya chukula
  • tatu baada ya kupata matumizi yako muhimu yanagharimu kiasi gani angalia unabakiwa na kiasi gani baada ya kufanya matumizi yako muhimu.
  • chukua kiasi kinachobaki kigawanye kwa uwiano sawa katika mafungu matatu yaani Akiba, Tahadhari/ dharura na Sadaka.
  • igawiye hiyo pesa bila kuajli ni kidogo kiasi gani kumbuka hicho ni kipato cha siku, fanya hivyo kila siku uendayo kufanya kazi halafu angalia baada ya mwisho wa wiki utakua umetunza kiasi gani na hiyo pia ni kwa wiki endelea kufanya hivyo kwa mwezi mzima hadi mwaka.
  • jiwekee malengo yako baada ya kugundua unapata kiasi gani kwa mwaka
  • malengo yako yaendane na kile unachofikiria kufanya au ambacho unaamini unaweza kufanya muda wowote kama atajitokeza mtu wa kuwezesha kufanya hivyo.
  • kwa kufanya hivyo utakuwa umejiwezesha bila kuwezeshwa na hakuna atakae amini mpaka umsimulie ni kwa jinsi gani umeweza kufanya hivyo.

kwa leo naomba niishie hapo kwa yeyote atakae kuwa na swali au oni anilize kupitia ukurasa huu wa GODFREY FREEDOMAN’S FUND au anitafute kwa mawasiliano ya simu ya mkononi +255 753 450 283/ +255 688 140 350 au E-Mail: godfreychacha45@gmail.com au tembelea blog yangu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com     

Nawatakia usomaji mwema Red rosewenye tafakari yakinifu na yenye kuzingatia yale ninayo wafundisha kwani ninaamini maneno yangu haya ni msaada tosha katika maisha yenu.

0 comments:

Post a Comment

kwa wale ambao wanapenda kuchangia au kutoa maoni ktika maada mbalimbali tunazokua tumetoa tafadhali zingatia maadili ya maada husika
usiende kinyume na utaratibu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yako.
mwisho niwatakie kila la heri na Mungu awabariki ktk kushiriki mambo mema ya ujenzi wa Taifa letu Tanzania.