Tuesday, 30 September 2014

MWENGE WA UHURU CHACHU YA UPIGAJI KURA YA MAONI RASIMU YA KAITIBA KWA WANANCHI

Mwenge wa uhuru uliwasili juzi jumapili ktk wilaya ya Chato ambapo mwenge huo ulizindua miradi mbalimbali ikiwemo ofisi ya Tarafa ya kachwamba na Stend kuu ya mabasi yaendayo mikoani na ndani ya wilaya chato awali wakati akiukabitdhi mwenge huo kaimu kiongozi wa mbio za mwenge taifa aliukabadhi kwa wanachi wa wilaya ya chato akisema kua kauli mbiu ya mwenge huo kwa mwaka wa 2014 ni kuwa mzalendo shiriki kupiga kura ya maoni ili kufanikisha upatikanaji wa katiba ya jumhuri ya muungano wa Tanzania; aidha wakati akiukaribasha mwenge huo ktk wilaya ya Chato mkuu wa wilaya ya Chato Ndg. Godrick Mpogoro aliwakaribisha viongozi wa mbio za mwenge na kutoa wosia kwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusema kuwa karibini chato kwa kushiriki ktk shughuli za maendeleo kwani wananchi wa wilaya ya chato ni wapenda maendeleo na chato ni ya amani pia nakuwasii wananchi kutumia mwenge kama fursa ya kuweza kutatua changamoto zinazowakabili ktk shughuli zao za maendeleo.











Hawa ni baadhi ya wanakwaya wa kwaya ya nyangomango walipokua wakitumbuiza katika ksherekea na kupokea mwenge wa uhuru.

0 comments:

Post a Comment

kwa wale ambao wanapenda kuchangia au kutoa maoni ktika maada mbalimbali tunazokua tumetoa tafadhali zingatia maadili ya maada husika
usiende kinyume na utaratibu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yako.
mwisho niwatakie kila la heri na Mungu awabariki ktk kushiriki mambo mema ya ujenzi wa Taifa letu Tanzania.