Pata makala zilizotokana na uchambuzi wa vitabu mbalimbali na shuhuda za maisha ya mafanikio ya watu mbalimbali. Makala hizi hakika zitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kuweka malengo na kufanyia kazi malengo yako kila siku mpaka pale unapofanikisha malengo yako.
Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja ana uchu wa mafanikio lakini wengi hushindwa kufikia mafanikio makubwa kwa kukosa kuwa na mipango sahihi ya kufanikisha malengo yao lakini kwa kukubali kuungana nami na kufanyia kazi yale utakayojifunza hapa kila siku za maisha yako hakika hutashindwa kufanikiwa.
Kumbuka "Debe tupu halikosi kelele" hivi ndivyo watu wanaoshindwa kufanikisha malengo yao walivyo hawakosi visingizio vya hapa na pale kumbe hawajui wao ni debe tupu wanacho hitaji ni kulijaza unga, unga ambao ni maarifa sahihi yanayoendana na malengo yao.
ujumbe wangu kuanzia sasa "Acha kuwa Debe tupu tafuta maarifa sahihi yatakayotatua changamoto za maisha yako"
0 comments:
Post a Comment
kwa wale ambao wanapenda kuchangia au kutoa maoni ktika maada mbalimbali tunazokua tumetoa tafadhali zingatia maadili ya maada husika
usiende kinyume na utaratibu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yako.
mwisho niwatakie kila la heri na Mungu awabariki ktk kushiriki mambo mema ya ujenzi wa Taifa letu Tanzania.