NJIA AMBAZO ZINALETA MAFANIKIO YA HARAKA KATIKA KUFANIKISHA MAISHA.
Katika mada zilizo pita tumeona ni kwa namna gani mtu anaweza kujikomboa na umasikini kwa kutumia, mazingira yake na pia kwa kutumia kipato chake yaani kwa namna nyingine tunaweza kusema kwa kutumia pesa inayopita mikononi mwake.
Tulizungumzia mambo mengi na ya msingi kabisa katika maisha halisi wa vijana wengi wa kitanzia ambao ndio tegemeo kubwa hasa katika shughuli zalishaji na maendeleo kwa ujumla kama ulikoswa unaweza kubonyeza haya mandishi www.facebook.com/godfreyfreedoman’fund au kutembelea blog yetu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com
Leo tutazungumzia njia mabazo ziweza kuleta mafanikio ya haraka katika kufanikisha maisha.Unapokuwa unatafuta maisha lazima ujiwekee malengo ambayo umeyapanga kuyafanikisha katika kipindi gani cha utafutaji wako kulingana na kipato ulichonacho kwa wakati huo. Na hii imewashinda vijana wengi kwani wamekuwa wakiweka malengo lakini baadae kuyatelekeza
mimi leo nimekuja kukushauri kamwe usiache kufanikisha lengo ambalo umelipanga kwa sababu labda unaona litakuchukuwa muda mrefu kulikamilisha na kunzisha lengo lingine ambalo unaamini litakuchukua muda mfupi kulikamilisha. Kwa kufanya hivi utakua unajirudisha nyuma bila wewe kujua ukumbuke kuwa muda mzuri wa kuweka malengo ni mwishini mwa mwaka au mwanzoni mwa mwaka baada ya kuwa umefanikisha baadhi ya malengo uliokuwa umepanga kuyafanikisha na katika hili inategemea emapanga kufanikisha maengo yako kwa kipindi gani kuna watu wanapanga malengo ya kila baada ya mwaka mmoja na wengine miaka miwili mpaka mitano na mimi leo nataka nikushirikishe baadhi ya njia mambazo natimia katika kupanga malengo yangu na naamini kama utazifuata utafiaka mbali katika kufanikisha malengo yako.
- kwanza unatakiwa uangalie mahitaji yako muhimu ambayo unapaswa kuwa nayo kama binadamu na moja ya mahitaji muhimi ya binadamu ambayo yanatajwa duniani kote ni haya yafuatayo:- Makazi, chakula na mavazi haya ni mahitaji ambayo wewe kama kijana unahitaji kuyapa kipaumbele kabla haujaanza mipango yako mingine ya kimaisha.
- pili ni kuyawekea mipango ya utekelezaji kimoja baada ya kingine au vyote kwa pamoja. malengo ya mipango ya utekelezaji wa mambo haya hauhitaji malengo mafupi kwani ndani ya utekelezaji wa malengo hayo kuna maisha mengine yanaendelea ikiwemo misukosuko ya hapa na pale kwa hiyo basi unatakiwa kuyawekea malengo marefu ambao utakupa nafasi nzuri ya kuyafanikisha ukumbuke kuwa huu ndiyo mwanzo wa utafutaji wako katika harakati za maisha na kama ukichelea hapo utashindwa kufanikisha malengo maengine mengi sana.
- tatu kuanza kubuni miradi ambayo itakusaidia kakamilsha utekelezaji wa maelngo uliojiwekea kwa kipindi hicho. kama wewe bado unaishi nyumbani na wazazi wako na huna kazi ya kufanya yaani ni tegemezi wa wazazi wako anza kuwaza kuwa baada ya hapo kuna majukumu ambayo yatakuhitaji hapo baadae kwa hiyo anza kufikiria namna ya kufanikisha pindi utakapoamua kufanya hivyo. nadhani unatambua unaweza kuwa tegemezi wa wazazi wako kipindi cha uhai wao tu na watakapo toweka au kuchoka kutafuta au utakapoamua kupata familia huo ndio utakuwa mwisho wa utaegemezi wako kwao na kama bado watakuwa hai na hawana nguvu za kutafuta tena itakubidi na wewe uwatunze kama walivyofanya kwako na kama utakuwa haijajipanga vizuri huu ndio utakuwa mwanzo wa ugumu wa maisha yako ambao unaweza ukakupoteza zaidi katika ramani za maisha nautafuataji.
- usiwe mtu wa kutaka kufanikisha kila wazo linalokwijia wakati ambao umeshapanga kutekeleza wazo lingine. namaanisha vijana wengi tumekuwa tukitamani kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ilihali tunajua kipato chetu halisi kilivyo sisemi kwamba usifanye mafanikio makubwa wakati kipato chako ni kidogo hapana nachokimaanisha ni kuepuka vishawishi vingi ambavyo vianaweza kukuvurugia mipango yako na kama unabisha ktk hili mimi nimeona wengi wakipotea katika ramani ya utafutaji kwa sababu ya kufuata vishaiwishi vya wenzao. mfano tuchulie wewe ni mwajiriwa wa serikali au taasisi fulani kipato chako kwa mwezi kinatosha kukidhi mahitaji yako kwa kipindi hicho cha mwezi mzima na ukabakiwa na balance ya kukutosha kufanya mambo mengine hebu fanya kwa kutumia hiyo balansi yako kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama nilivyotangulia kusema kwenye maelezo yangu ya mwanzo, usikubali kushawishika kufanya jambo ambalo hukulipangilia ila tu kwa sababu umeambiwa na rafiki yako wakati hukupanga kulifanya jambo hili, kwa kufanya hivyo utakua umaharibu mipango yako na umeingilia mipango yako kama umembiwa jambo na mtu na jambo lile hukulipangilia kulifanya na ukaliona jambo hilo ni zuri ni vyema ukaliweka kwenye mipango yako ya baadae na si kulifanya liharibu mipango yako na kwa kufanya hivyo litakupa muda mzuri wa kulifanyia utafiti kama kweli linafaa.
kwa kutumia mbinu hizo na nyingine nyingi ambazo sikuzitaja hapo unaweza kufanikisha malengo yako kwa wakati uliojipangia na kama utakuahaujafanikisha yote utakuwa kwa kiasi fulani umepata mwelekeo wa kufanikisha malengo yako na hivyo basi itakutia moyo wa kuendeleza utekelezaji wa mipango yako siku hadi siku na utapata nafasi ya kuongeza mipango mingine kila baada ya kukamilisha mpango moja aumiwili.
mada yetu ya leo imelenga kuongelea njia mbalimbali ambazo zinaweza kuleta mafanikio ya maisha lakini katika upana wa mada hii tumweza kuzungumzia hayo machache na mimi sipendi niwachoshe wasomaji wangu bali mpate kidogo kitakachowapa tafakari juu ya kile nilichokiongelea. kwa leo naomba niishie hapo nikipata muda nitakuja kuwaelezea mbinu hizo kinagaubaga ambazo moja ya mbinu kuu ni ushirikiano wa pamoja katika kufanikisha maisha mmoja baada ya mwingine.
Ahsanteni sana kwa kunifutilia juu ya kile nachokiongelea ambapo mimi naamini hata usiponielewa leo lakini ukiendelea kunifuatilia utajua nini nachokiongelea na kina msada gani katika maisha yako ya leo,kesho na kesho kutwa kwa hiyo ni kusihi tu endelea kunifuatilia hata kama hunielewi kwani ipo siku utanielewa.