Vinywaji baridi

Wakazi wa Chato, kwa mahitaji ya vinywaji Baridi fika Kwa shambani Maeneo ya Stendi ya zamani ujipatie mahitaji yako kwa Bei ya Jumla na rejreja

Networking

Kwa mahitaji ya Network Etup, Network Configuration and troubleshooting waone WAMICO ukiwa Mjini chato wapo Stendi mpya ya mabasi Muungano

Friday, 10 June 2016

GODFREY FREEDOMAN’S FUND

NJIA AMBAZO ZINALETA MAFANIKIO YA HARAKA KATIKA KUFANIKISHA MAISHA.High fiveSnapShot(4)SnapShot(4)

Katika mada zilizo pita tumeona ni kwa namna gani mtu anaweza kujikomboa na umasikini kwa kutumia, mazingira yake na pia kwa kutumia kipato chake yaani kwa namna nyingine tunaweza kusema kwa kutumia pesa inayopita mikononi mwake.

Tulizungumzia mambo mengi na ya msingi kabisa katika maisha halisi wa vijana wengi wa kitanzia ambao ndio tegemeo kubwa hasa katika shughuli zalishaji na maendeleo kwa ujumla kama ulikoswa unaweza kubonyeza haya mandishi www.facebook.com/godfreyfreedoman’fund  au kutembelea blog yetu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com

Leo tutazungumzia njia mabazo ziweza kuleta mafanikio ya haraka katika kufanikisha maisha.Unapokuwa unatafuta maisha lazima ujiwekee malengo ambayo umeyapanga kuyafanikisha katika kipindi gani cha utafutaji wako kulingana na kipato ulichonacho kwa wakati huo. Na hii imewashinda vijana wengi kwani wamekuwa wakiweka malengo lakini baadae kuyatelekeza

mimi leo nimekuja kukushauri kamwe usiache kufanikisha lengo ambalo umelipanga kwa sababu labda unaona litakuchukuwa muda mrefu kulikamilisha na kunzisha lengo lingine ambalo unaamini litakuchukua muda mfupi kulikamilisha. Kwa kufanya hivi utakua unajirudisha nyuma bila wewe kujua ukumbuke kuwa muda mzuri wa kuweka malengo ni mwishini mwa mwaka au mwanzoni mwa mwaka baada ya kuwa umefanikisha baadhi ya malengo uliokuwa umepanga kuyafanikisha na katika hili inategemea emapanga kufanikisha maengo yako kwa kipindi gani kuna watu wanapanga malengo ya kila baada ya mwaka mmoja na wengine miaka miwili mpaka mitano na mimi leo nataka nikushirikishe baadhi ya njia mambazo natimia katika kupanga malengo yangu na naamini kama utazifuata utafiaka mbali katika kufanikisha malengo yako.

  1. kwanza unatakiwa uangalie mahitaji yako muhimu ambayo unapaswa kuwa nayo kama binadamu na moja ya mahitaji muhimi ya binadamu ambayo yanatajwa duniani kote ni haya yafuatayo:- Makazi, chakula na mavazi haya ni mahitaji ambayo wewe kama kijana unahitaji kuyapa kipaumbele kabla haujaanza mipango yako mingine ya kimaisha.
  2. pili ni kuyawekea mipango ya utekelezaji kimoja baada ya kingine au vyote kwa pamoja. malengo ya mipango ya utekelezaji wa mambo haya hauhitaji malengo mafupi kwani ndani ya utekelezaji wa malengo hayo kuna maisha mengine yanaendelea ikiwemo misukosuko ya hapa na pale kwa hiyo basi unatakiwa kuyawekea malengo marefu ambao utakupa nafasi nzuri ya kuyafanikisha ukumbuke kuwa huu ndiyo mwanzo wa utafutaji wako katika harakati za maisha na kama ukichelea hapo utashindwa kufanikisha malengo maengine mengi sana.
  3.   tatu kuanza kubuni miradi ambayo itakusaidia kakamilsha utekelezaji wa maelngo uliojiwekea kwa kipindi hicho. kama wewe bado unaishi nyumbani na wazazi wako na huna kazi ya kufanya yaani ni tegemezi wa wazazi wako anza kuwaza kuwa baada ya hapo kuna majukumu ambayo yatakuhitaji hapo baadae kwa hiyo anza kufikiria namna ya kufanikisha pindi utakapoamua kufanya hivyo. nadhani unatambua unaweza kuwa tegemezi wa wazazi wako kipindi cha uhai wao tu na watakapo toweka au kuchoka kutafuta au utakapoamua kupata familia huo ndio utakuwa mwisho wa utaegemezi wako kwao na kama bado watakuwa hai na hawana nguvu za kutafuta tena itakubidi na wewe uwatunze kama walivyofanya kwako na kama utakuwa haijajipanga vizuri huu ndio utakuwa mwanzo wa ugumu wa maisha yako ambao unaweza ukakupoteza zaidi katika ramani za maisha nautafuataji.
  4. usiwe mtu wa kutaka kufanikisha kila wazo linalokwijia wakati ambao umeshapanga kutekeleza wazo lingine. namaanisha vijana wengi tumekuwa tukitamani kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ilihali tunajua kipato chetu halisi kilivyo sisemi kwamba usifanye mafanikio makubwa wakati kipato chako ni kidogo hapana nachokimaanisha ni kuepuka vishawishi vingi ambavyo vianaweza kukuvurugia mipango yako na kama unabisha ktk hili mimi nimeona wengi wakipotea katika ramani ya utafutaji kwa sababu ya kufuata vishaiwishi vya wenzao. mfano tuchulie wewe ni mwajiriwa wa serikali au taasisi fulani kipato chako kwa mwezi kinatosha kukidhi mahitaji yako kwa kipindi hicho cha mwezi mzima na ukabakiwa na balance ya kukutosha kufanya mambo mengine hebu fanya kwa kutumia hiyo balansi yako kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama nilivyotangulia kusema kwenye maelezo yangu ya mwanzo, usikubali kushawishika kufanya jambo ambalo hukulipangilia ila tu kwa sababu umeambiwa na rafiki yako wakati hukupanga kulifanya jambo hili, kwa kufanya hivyo utakua umaharibu mipango yako na umeingilia mipango yako kama umembiwa jambo na mtu na jambo lile hukulipangilia kulifanya na ukaliona jambo hilo ni zuri ni vyema ukaliweka kwenye mipango yako ya baadae na si kulifanya liharibu mipango yako na kwa kufanya hivyo litakupa muda mzuri wa kulifanyia utafiti kama kweli linafaa.

kwa kutumia mbinu hizo na nyingine nyingi ambazo sikuzitaja hapo unaweza kufanikisha malengo yako kwa wakati uliojipangia na kama utakuahaujafanikisha yote utakuwa kwa kiasi fulani umepata mwelekeo wa kufanikisha malengo yako na hivyo basi itakutia moyo wa kuendeleza utekelezaji wa mipango yako siku hadi siku na utapata nafasi ya kuongeza mipango mingine kila baada ya kukamilisha mpango moja aumiwili.

mada yetu ya leo imelenga kuongelea njia mbalimbali ambazo zinaweza kuleta mafanikio ya maisha lakini katika upana wa mada hii tumweza kuzungumzia hayo machache na mimi sipendi niwachoshe wasomaji wangu bali mpate kidogo kitakachowapa tafakari juu ya kile nilichokiongelea. kwa leo naomba niishie hapo nikipata muda nitakuja kuwaelezea mbinu hizo kinagaubaga ambazo moja ya mbinu kuu ni ushirikiano wa pamoja katika kufanikisha maisha mmoja baada ya mwingine.

Red roseAhsanteni sana kwa kunifutilia juu ya kile nachokiongelea ambapo mimi naamini hata usiponielewa leo lakini ukiendelea kunifuatilia utajua nini nachokiongelea na kina msada gani katika maisha yako ya leo,kesho na kesho kutwa kwa hiyo ni kusihi tu endelea kunifuatilia hata kama hunielewi kwani ipo siku utanielewa. SnapShot(4)

Monday, 6 June 2016

GODFREY FREEDOMAN’S FUND

High fiveMWENDELEZO WA MPANGO WA KUHAKIKISHA KIJANA ANAJITEGEMEA KATIKA MASWALA YA KIUCHUMI NA MAISHA KWA UJUMLA:

GODFREY FREEDOMAN’S FOUNDATION katika kuhakikisha kuwa kijana anchukuwa nafasi yake ya chachu katika jamii hasa katika maswala ya kiuchimi na maisha kwa ujumla inendeleza harakati zake za kuendelea kuhamasisha vijana ili waendelee kutumia nafasi walizonazo kama fursa ya kujikomboa na umasikini na kuudhihirishia umma kuwa kijana ni chachu ya maendeleo katika Taifa lolote lile. Hivyo basi katika mada iliyopita tuliona ni kwa namna gani kijana anayeishi kijijini anavyoweza kujikomboa na umasikini kwa kutumia mazingira yake bila hata ya kusafiri kwa ajili ya kutafuata maisha. Leo pia tunaendelea na mada yetu hasa kwa vijana waoishi mijini, mara nyingi tumekuwa tikisistizwa kufanya kazi kwa bidii ili tuondokane na umasikini lakini hatujui kuwa kufanya kazi tu haitoshi bali kufanya kazi kwa kujiwekea malengo ndiyo swala muhimu katiaka swala zima la ufanikishaji wa maisha. vijana wengi tumekuwa tukifanya kazi lakini hatuthamini kipato tunachopata kutokana na kazi hiyo kwani  tumekuwa tukidhani kuwa kipato tunachopata ni kidogo sana hivyo basi kinatutosheleza kufanya mahitaji madogomadogo tu jambo ambalo sio la kweli. Sawa kipato chetu ni kidogo na kinatosha mahitaji madogomadogo lakini sas hebu tumia hicho kidogo unachopata ili kutafuta kikubwa ambacho wewe unakihitaji. Mfano tuchukulie   wewe ni kinyozi, kibarua, mpiga debe, bodaboda, daladala (mwendesha baiskeli), muuzaji wa bidhaa ndogondogo yaani karanga, pipi maji n,k. Hapa nataka kuongea hawa watu ni kwanamna gani wanaweza kuwa matajiri kwa kutumia kaipato cha kazi zao bila ya kuwezeshwa na mtu mwingine ila tu kwa kutegemea kipato chao na huku maisha yanendelea. najua wengi mtaniuliza mwendesha baiskeli atawezaje kupata pesa ya kumfanya aache kuendesha baiskeli wakati gharama wanazobebea abiria ni kidogo saana kiasi kwamba pengine hazitoshi kukidhi mahitaji ya siku ktk familia mimi nasema si kweli kwani hakuna mtu anayeweza kufanya kazi ambayo haiwezi kumwezesha hata kupata mlo wa siku moja na kama unaamini hivyo jiulize kama haimwezeshi kupata mlo hata wa siku moja anapata wapi chakula kinachompa nguvu ya kuja kufanya kazi, tena kazi ngumu? Nachotaka nikushauri wewe ambae uko katika hili hizo nilizozitaja hapo juu unachotakiwa kufanya ni kunzingatia yafuatayo:-

  • kwanza kabisa angalia unapta shilingi ngapi baada ya mizunguko yako ya siku.
  • pili angalia matumazi yako muhimu ya siku yanagharimu shilingi ngapi. Napozungumzia mahitaji muhimu nina maanisha mahitaji ya chukula
  • tatu baada ya kupata matumizi yako muhimu yanagharimu kiasi gani angalia unabakiwa na kiasi gani baada ya kufanya matumizi yako muhimu.
  • chukua kiasi kinachobaki kigawanye kwa uwiano sawa katika mafungu matatu yaani Akiba, Tahadhari/ dharura na Sadaka.
  • igawiye hiyo pesa bila kuajli ni kidogo kiasi gani kumbuka hicho ni kipato cha siku, fanya hivyo kila siku uendayo kufanya kazi halafu angalia baada ya mwisho wa wiki utakua umetunza kiasi gani na hiyo pia ni kwa wiki endelea kufanya hivyo kwa mwezi mzima hadi mwaka.
  • jiwekee malengo yako baada ya kugundua unapata kiasi gani kwa mwaka
  • malengo yako yaendane na kile unachofikiria kufanya au ambacho unaamini unaweza kufanya muda wowote kama atajitokeza mtu wa kuwezesha kufanya hivyo.
  • kwa kufanya hivyo utakuwa umejiwezesha bila kuwezeshwa na hakuna atakae amini mpaka umsimulie ni kwa jinsi gani umeweza kufanya hivyo.

kwa leo naomba niishie hapo kwa yeyote atakae kuwa na swali au oni anilize kupitia ukurasa huu wa GODFREY FREEDOMAN’S FUND au anitafute kwa mawasiliano ya simu ya mkononi +255 753 450 283/ +255 688 140 350 au E-Mail: godfreychacha45@gmail.com au tembelea blog yangu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com     

Nawatakia usomaji mwema Red rosewenye tafakari yakinifu na yenye kuzingatia yale ninayo wafundisha kwani ninaamini maneno yangu haya ni msaada tosha katika maisha yenu.

Wednesday, 18 May 2016

GODFREY FREEDOMAN’S FUND

GODFREY FREEDOMAN’S FUND ni mpango unaolenga kuinua na kukuza uchumi/kipato cha kijana wa kitanzania. mpango huu ulianza kwa kuwalenga vijana wa wilaya ya Rorya mkoani Mara hasa kwa kata ya Kisumwa na vitongoji vyake, ambao mimi Godfrey chacha kama kijana wa jamii hiyo ya watu wa Rorya nilikaa nikatathmini miasha halisi ya sisi vijana nikaona kuna haja ya kushirikisha mawazo,ushauri,na kuelimishana ni kwa namna gani tunaweza tukajikomboa na umasikini ukizingatia familia zetu kwa kiasi kikubwa tuishi katika hali ya umasikini. Hivyo basi kwa kuzingatia mazingira tunaishi nikaona ndio nguzo itakayo tuwezesha kujikomboa na janga hili endapo tutayatumia vizuri, ninaposema “tutayatumia vizuri” simanishi tunayatumia mazingira yetu vibaya hapana nachokimanisha hapa ni kuchukua mazingira tulionayo kama fursa ya kutukomboa na umasikini sio kifikiria kutoka kwenda kutafuta maisha mazuri sehemu nyingine bali tutumie ule msemo wa kiswahili usemao “Chako ndio kinakusaidia”. sasa basi tutumieje chetu tulichonacho kijikomboa na umasikini?

kwa kuzingatia hali ya hewa ya mkoa wa Mara kwa ujumla tunapata misimu miliya ya mvua ambayo inatuwezesha kulima na kuvuna mazo ya kutosha kwa misimu yote miwili. Hivyo basi tulime sana lakini tulime kwa kuzingatia kilimo bora yaani ninaposema kilimo bora namaanisha kulima kwa kufuata kanuni za kilimo cha kisasa tuondokane na kilimo cha kizamani na tofauti kati ya kilimo cha kisasa na kilimo cha kizamani ni hizi hapa:-

1. kilimo cha kisasa kinahitaji uandae shamba mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha sio kama tulivyo zoe mara nyingi tunandaa mashamba wakati mvua zimeanza jambo ambalo linatupelekea kulima tukiwa tumechelewa na mvua kukatika kabla mazao yetu hayajakomaa ikumbkwe kuwa mvua hizi ni za msimu sio za muda wote hivyo basi ni vyema kutambua majira ya mvua hizi kwa ajili ya maandalizi ya kilimo.

2. kilimo cha kisasa kinahitaji shamba liwe na rutuba ya kutosha kwa ajili ya kupata mazao mengi. mara nyingi tumekuwa tukilima tu shamba miaka nenda rudi bila hata kujali je rutuba ya shamba hili bado ni nzuri kwa ajilli ya kimo cha zao unalolima hivyo basi moja ya maandalizi ya shamba mojawapo ya kuhakikisha ni kwamba shamba unaloliandaa lina rutuba ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha mazao kama halina unaweza kiliongeazea kwa kuweka mbolea ya asili au mbolea inayouzwa madukani

3. kupanda begu bora ambazo zitaota vizuri na kutupelekea kuvuna mazo mengi. bengu bora ni zile zinazopatikana madukani na si kwingineneko mara nyingi tumekuwa tukipanda mbegu ambazo tunakua tumetunza au kunua zile ambazo zimepelekwa sokoni aidha kwa ajili ya chakula mbegu hizi sio bora kitaalam maana sio zote zinazoota ukipanda kwa hiyo hupelekea kuacha nafasi wazi sehemu ya shamba  ambayo wakati mwingine inatulazimu kurudia kupanda upya.

4. kupanda kwa kufuata utaalamu wa upandaji ni, ni vyema ukamshirikisha mtaalamu wa kilimo hasa maafisa wa kilimo kwa ajili ya kukuelekeza namna ya ubandaji ambao utakuwezesha kupata mazao bora.

Hizo ndizo moja ya tofauti za kilimo cha kisasa na kilimo cha zamani na nyinginezo nyingi. Baada ya kujiakikishia kilimo bora na mavuno ya kutosha inatupaswa kutumia vyema mavuno tuliopata ili kuendelea kujiimarisha kuichumi na kimaendeleo zaidi.

Tuanayatumiaje mavuno yetu vyema ili tuweze tuweze kujiimarisha kiuchumi?

1. ni kuhakikisha tunapata soko la uhakika la mazao yetu, soko ambalo lina maslai makubwa kwetu sisi wakulima na sio wafanya biashara au wanunuzi wa mazao yetu,wote tunatakiwa kunufaiki kila mmoja kwa nafasi yake kwa namna hiyo basi inapaswa tushirikiane na serikali yetu katika kuuza mazao yetu kwani yenyewe ndiyo itakayo tusaidia kuuza mazao yetu bila ya kunyanyaswa.

2. baada ya kuuza mazao yetu tutumie vyeama pesa tuliopata. Kila mmoja awe na malengo juu pesa aliyopata, na moja ya malengo ambayo kila mmoja atayaweka katika akili yake juu ya pesa anayopata kutokana na kilimo ni kama ifuatavyo kujenga nymba bora, kuhakikisha watoto wanakwenda shule na kupata elimu bora kubuni miradi mbalimbali ambayo itamhakikishia kipato hata bila ya kulima.

Haya ndiyo yalikuwa malengo ya Godfrey chacha wakati anabuni huo mpango wa GODFREY FREEDOMAN’S FUND nikilenga kujikomboa na kuwakombo vijana wenzangu hasa wa jamii hii ya mkoa wa Mara lakini nikaona Dunia sasa imekuwa kijiji kwa nini mpango huu nisiwashirikishe vijana wote wa kitanzania ambao naamini adha yetu ni moja? kwa kufanya hivyo nikaleta swala hili kwenu Watanzania wenzangu tena wachapa kazi tuachane na dhana ya kusema kwa sisi ni masikini kwa sababu Taifa letu ni masikini mimi nasema sisi si masikini na Taifa letu si masikini ila tu tushiriki kufanya kazi na viongozi wetu pia washiriki vyema kusimamia kazi zetu na kutupa sapoti pindi tunapohitaji msaada wao aidha wa kimawazo, uwezeshaji na mabo mengine mengi.

tumeona hapo juu nimejaribu kungumzia ni namna gani jamii wa watu wa msoma wanaweza kujikwamua kotokana na umasikini wao kwa njia kilimo kulingana na mazingira yao je wewe kijana unaeishi mjini na huna sehemu ya kulima utafanyaje? je ufunge safari uende kijijini kukalime? au uendelee kutafuta maeneo ya wazi yalioko mjini ukalime hapana majibu ya maswali haya tutayapata kitika somo lijalo cha msingi ni kukaa makini na kuendelea kunifuatilia katika ukurasa wangu wa facebook kwa kutafuta GODFREY FREEDOMAN’S FUND au kutembelea blog yangu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com au E-Mail: godfreychacha45@gmail.com au piga simu No. 0753 450 283 /0688 140 350.