Vinywaji baridi

Wakazi wa Chato, kwa mahitaji ya vinywaji Baridi fika Kwa shambani Maeneo ya Stendi ya zamani ujipatie mahitaji yako kwa Bei ya Jumla na rejreja

Networking

Kwa mahitaji ya Network Etup, Network Configuration and troubleshooting waone WAMICO ukiwa Mjini chato wapo Stendi mpya ya mabasi Muungano

Wednesday, 18 May 2016

GODFREY FREEDOMAN’S FUND

GODFREY FREEDOMAN’S FUND ni mpango unaolenga kuinua na kukuza uchumi/kipato cha kijana wa kitanzania. mpango huu ulianza kwa kuwalenga vijana wa wilaya ya Rorya mkoani Mara hasa kwa kata ya Kisumwa na vitongoji vyake, ambao mimi Godfrey chacha kama kijana wa jamii hiyo ya watu wa Rorya nilikaa nikatathmini miasha halisi ya sisi vijana nikaona kuna haja ya kushirikisha mawazo,ushauri,na kuelimishana ni kwa namna gani tunaweza tukajikomboa na umasikini ukizingatia familia zetu kwa kiasi kikubwa tuishi katika hali ya umasikini. Hivyo basi kwa kuzingatia mazingira tunaishi nikaona ndio nguzo itakayo tuwezesha kujikomboa na janga hili endapo tutayatumia vizuri, ninaposema “tutayatumia vizuri” simanishi tunayatumia mazingira yetu vibaya hapana nachokimanisha hapa ni kuchukua mazingira tulionayo kama fursa ya kutukomboa na umasikini sio kifikiria kutoka kwenda kutafuta maisha mazuri sehemu nyingine bali tutumie ule msemo wa kiswahili usemao “Chako ndio kinakusaidia”. sasa basi tutumieje chetu tulichonacho kijikomboa na umasikini?

kwa kuzingatia hali ya hewa ya mkoa wa Mara kwa ujumla tunapata misimu miliya ya mvua ambayo inatuwezesha kulima na kuvuna mazo ya kutosha kwa misimu yote miwili. Hivyo basi tulime sana lakini tulime kwa kuzingatia kilimo bora yaani ninaposema kilimo bora namaanisha kulima kwa kufuata kanuni za kilimo cha kisasa tuondokane na kilimo cha kizamani na tofauti kati ya kilimo cha kisasa na kilimo cha kizamani ni hizi hapa:-

1. kilimo cha kisasa kinahitaji uandae shamba mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha sio kama tulivyo zoe mara nyingi tunandaa mashamba wakati mvua zimeanza jambo ambalo linatupelekea kulima tukiwa tumechelewa na mvua kukatika kabla mazao yetu hayajakomaa ikumbkwe kuwa mvua hizi ni za msimu sio za muda wote hivyo basi ni vyema kutambua majira ya mvua hizi kwa ajili ya maandalizi ya kilimo.

2. kilimo cha kisasa kinahitaji shamba liwe na rutuba ya kutosha kwa ajili ya kupata mazao mengi. mara nyingi tumekuwa tukilima tu shamba miaka nenda rudi bila hata kujali je rutuba ya shamba hili bado ni nzuri kwa ajilli ya kimo cha zao unalolima hivyo basi moja ya maandalizi ya shamba mojawapo ya kuhakikisha ni kwamba shamba unaloliandaa lina rutuba ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha mazao kama halina unaweza kiliongeazea kwa kuweka mbolea ya asili au mbolea inayouzwa madukani

3. kupanda begu bora ambazo zitaota vizuri na kutupelekea kuvuna mazo mengi. bengu bora ni zile zinazopatikana madukani na si kwingineneko mara nyingi tumekuwa tukipanda mbegu ambazo tunakua tumetunza au kunua zile ambazo zimepelekwa sokoni aidha kwa ajili ya chakula mbegu hizi sio bora kitaalam maana sio zote zinazoota ukipanda kwa hiyo hupelekea kuacha nafasi wazi sehemu ya shamba  ambayo wakati mwingine inatulazimu kurudia kupanda upya.

4. kupanda kwa kufuata utaalamu wa upandaji ni, ni vyema ukamshirikisha mtaalamu wa kilimo hasa maafisa wa kilimo kwa ajili ya kukuelekeza namna ya ubandaji ambao utakuwezesha kupata mazao bora.

Hizo ndizo moja ya tofauti za kilimo cha kisasa na kilimo cha zamani na nyinginezo nyingi. Baada ya kujiakikishia kilimo bora na mavuno ya kutosha inatupaswa kutumia vyema mavuno tuliopata ili kuendelea kujiimarisha kuichumi na kimaendeleo zaidi.

Tuanayatumiaje mavuno yetu vyema ili tuweze tuweze kujiimarisha kiuchumi?

1. ni kuhakikisha tunapata soko la uhakika la mazao yetu, soko ambalo lina maslai makubwa kwetu sisi wakulima na sio wafanya biashara au wanunuzi wa mazao yetu,wote tunatakiwa kunufaiki kila mmoja kwa nafasi yake kwa namna hiyo basi inapaswa tushirikiane na serikali yetu katika kuuza mazao yetu kwani yenyewe ndiyo itakayo tusaidia kuuza mazao yetu bila ya kunyanyaswa.

2. baada ya kuuza mazao yetu tutumie vyeama pesa tuliopata. Kila mmoja awe na malengo juu pesa aliyopata, na moja ya malengo ambayo kila mmoja atayaweka katika akili yake juu ya pesa anayopata kutokana na kilimo ni kama ifuatavyo kujenga nymba bora, kuhakikisha watoto wanakwenda shule na kupata elimu bora kubuni miradi mbalimbali ambayo itamhakikishia kipato hata bila ya kulima.

Haya ndiyo yalikuwa malengo ya Godfrey chacha wakati anabuni huo mpango wa GODFREY FREEDOMAN’S FUND nikilenga kujikomboa na kuwakombo vijana wenzangu hasa wa jamii hii ya mkoa wa Mara lakini nikaona Dunia sasa imekuwa kijiji kwa nini mpango huu nisiwashirikishe vijana wote wa kitanzania ambao naamini adha yetu ni moja? kwa kufanya hivyo nikaleta swala hili kwenu Watanzania wenzangu tena wachapa kazi tuachane na dhana ya kusema kwa sisi ni masikini kwa sababu Taifa letu ni masikini mimi nasema sisi si masikini na Taifa letu si masikini ila tu tushiriki kufanya kazi na viongozi wetu pia washiriki vyema kusimamia kazi zetu na kutupa sapoti pindi tunapohitaji msaada wao aidha wa kimawazo, uwezeshaji na mabo mengine mengi.

tumeona hapo juu nimejaribu kungumzia ni namna gani jamii wa watu wa msoma wanaweza kujikwamua kotokana na umasikini wao kwa njia kilimo kulingana na mazingira yao je wewe kijana unaeishi mjini na huna sehemu ya kulima utafanyaje? je ufunge safari uende kijijini kukalime? au uendelee kutafuta maeneo ya wazi yalioko mjini ukalime hapana majibu ya maswali haya tutayapata kitika somo lijalo cha msingi ni kukaa makini na kuendelea kunifuatilia katika ukurasa wangu wa facebook kwa kutafuta GODFREY FREEDOMAN’S FUND au kutembelea blog yangu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com au E-Mail: godfreychacha45@gmail.com au piga simu No. 0753 450 283 /0688 140 350.

Monday, 24 November 2014

NGOMA YA ASILI

Kwa wale ambao wanaifahamu hii ngoma nadhani wakiiona watatamani niachie vidio wacheze ama wasikilize likini si kusudio langu lango ni kutaka kuufahamisha uma wa watanzania kuwa tunatakiwa kuuthamini uatamaduni wetu na kuutangaza pia

music


Tuesday, 30 September 2014

Hii ndiyo Tarime tunayoizungumzia na kutaka serikali kuingalia na kuitambua kama sehemu ya pato la taifa kwa sababu ya uzalishaji wake wa chakula cha kutosha na madini aina ya dhahabu karibu eneo lote la tarime na wilaya jirani ya Rorya na pia inasadikika kuwa ndani ya wilaya ya Rorya kuna madini aina ya urenium ambayo serikali haijafika kuyafanyia utafiti ili kubaini na wananchi waweze kunufaika na madini hayo hata hivyo tunaamini kuwa serikali inatambua kuwa wilaya ya Tarime na Rorya ni wilaya ambazo ukanda wa ke ni ukanda wa ikweta kwa hiyo wilaya hizi zinaweza kuzalisha chakula cha kutosha kama wananchi watawezeshwa na kuelimishwa zaidi ni mazao gani wanatakiwa kulima ili waweze kundokana na adha ya umaskini inayowakumba wananchi hao licha ya kuishi ktk ardhi ambayo ina rutuba na uwezekano mkubwa wa kuzalisha chakula.

UTAMADUNI NI SEHEMU YA KUJENGA MAADILI KWA VIJANA WA KITANZANIA

Kama ilivyozoeleka kwa  maadili ya sasa mtu kuzingztia na kufuatilia kanuni na tamaduni za kwao kwa vijana wa leo ni ushamaba kuonekana kwa kutoelimika au kutokukubali mabadiliko jamabo ambalo si kweli kabisa kwani kwa kukubali mabadiliko hayo tunashudia vijana wa sasa wanajikuta kupoteza na kupotea kabisa ktk swala zima la kushiriki ktk kutoa mchango wa aidha mawazo au maendeleo katika jamii jambo ambalo si halali ukizingatia kijana ndio chachu ya maendeleo ktk jamii yoyote ile kwa hiyo jambo hili haliitaji wazee kishiriki moja kwa moja ktk kuhamasisha vijana ktk kuzingatia na kufuata tamaduni za kwao bali ni vijana wenyewe wanatakiwa kujitathmini kuwa wao ni nani na nini wanatakiwa wafanye ili na wao waweze kushiriki moja kwa moja ktk mchango mzima wa maendeleo.
   kwa hali hiyo basi nachukua nafasi hii mimi kama kijana kuwasii vijana wenzangu kutambu kuwa sisi ndio chachu ya maendeleo inatupasa kujitahidi katika hili na ni ninaamini kuwa utakubaliana na mimi katika hili kuwa vijana bado hatushiririki moja kwa moja na badala yake wazee ndo wanahangaika huku na kule huku wakitutafutaia riziki wakati sisi vijana tukibaki kuvaa na kupendeza eti tunasema tunakula ujana acha hizo fikira unakula ujana wewe ni mstafu? au unakula ujana hizo pesa umezipata lini na umezipataje shirikisha wenzako ndoyo useme unakula ujana au anakula ujana kupitia mzazi wako je siku akitoka utakuala ujana wa nani yako kama si kuiba ama kuishia kuvuta bangi na kutumia madawa mengine ya kulevya achana na hizo fikira fupi bwana dunia ya sasa si yajana.

MWENGE WA UHURU CHACHU YA UPIGAJI KURA YA MAONI RASIMU YA KAITIBA KWA WANANCHI

Mwenge wa uhuru uliwasili juzi jumapili ktk wilaya ya Chato ambapo mwenge huo ulizindua miradi mbalimbali ikiwemo ofisi ya Tarafa ya kachwamba na Stend kuu ya mabasi yaendayo mikoani na ndani ya wilaya chato awali wakati akiukabitdhi mwenge huo kaimu kiongozi wa mbio za mwenge taifa aliukabadhi kwa wanachi wa wilaya ya chato akisema kua kauli mbiu ya mwenge huo kwa mwaka wa 2014 ni kuwa mzalendo shiriki kupiga kura ya maoni ili kufanikisha upatikanaji wa katiba ya jumhuri ya muungano wa Tanzania; aidha wakati akiukaribasha mwenge huo ktk wilaya ya Chato mkuu wa wilaya ya Chato Ndg. Godrick Mpogoro aliwakaribisha viongozi wa mbio za mwenge na kutoa wosia kwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusema kuwa karibini chato kwa kushiriki ktk shughuli za maendeleo kwani wananchi wa wilaya ya chato ni wapenda maendeleo na chato ni ya amani pia nakuwasii wananchi kutumia mwenge kama fursa ya kuweza kutatua changamoto zinazowakabili ktk shughuli zao za maendeleo.











Hawa ni baadhi ya wanakwaya wa kwaya ya nyangomango walipokua wakitumbuiza katika ksherekea na kupokea mwenge wa uhuru.

Saturday, 27 September 2014

HAPPY BIRTH DAY 













Wednesday, 24 September 2014

HOME
Haya ni baadhi ya maeneo yanayopatikana hapa kwetu tanzania na yanatuletea kipato kinachochangia sehemu ya pato la taifa japo hayasimamiwi ipaswavyo na hatimaye kuishia kwenye mikono ya watu ambao si wapenda maendeleo kwenye Taifa letu

Sunday, 31 August 2014

KISUMWA ROAD
karibu kisumwa ujionee maajabu na uzuri wa kisumwa si kuisikia tu kwa watu wakisimulia bana fika mwenyewe ujionee hapana chezea kisumwa wewe
Unapozungumzia kisumwa hii ndio Kisumwa tunayoizungumzia na si vinginevyo

Kwa wapenzi wote wa blog hii waweza kualika mtu yeyote na kumwambia atafute kwa kuungana nasi au kwa maoni na ushauri