GODFREY FREEDOMAN’S FUND ni mpango unaolenga kuinua na kukuza uchumi/kipato cha kijana wa kitanzania. mpango huu ulianza kwa kuwalenga vijana wa wilaya ya Rorya mkoani Mara hasa kwa kata ya Kisumwa na vitongoji vyake, ambao mimi Godfrey chacha kama kijana wa jamii hiyo ya watu wa Rorya nilikaa nikatathmini miasha halisi ya sisi vijana nikaona kuna haja ya kushirikisha mawazo,ushauri,na kuelimishana ni kwa namna gani tunaweza tukajikomboa na umasikini ukizingatia familia zetu kwa kiasi kikubwa tuishi katika hali ya umasikini. Hivyo basi kwa kuzingatia mazingira tunaishi nikaona ndio nguzo itakayo tuwezesha kujikomboa na janga hili endapo tutayatumia vizuri, ninaposema “tutayatumia vizuri” simanishi tunayatumia mazingira yetu vibaya hapana nachokimanisha hapa ni kuchukua mazingira tulionayo kama fursa ya kutukomboa na umasikini sio kifikiria kutoka kwenda kutafuta maisha mazuri sehemu nyingine bali tutumie ule msemo wa kiswahili usemao “Chako ndio kinakusaidia”. sasa basi tutumieje chetu tulichonacho kijikomboa na umasikini?
kwa kuzingatia hali ya hewa ya mkoa wa Mara kwa ujumla tunapata misimu miliya ya mvua ambayo inatuwezesha kulima na kuvuna mazo ya kutosha kwa misimu yote miwili. Hivyo basi tulime sana lakini tulime kwa kuzingatia kilimo bora yaani ninaposema kilimo bora namaanisha kulima kwa kufuata kanuni za kilimo cha kisasa tuondokane na kilimo cha kizamani na tofauti kati ya kilimo cha kisasa na kilimo cha kizamani ni hizi hapa:-
1. kilimo cha kisasa kinahitaji uandae shamba mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha sio kama tulivyo zoe mara nyingi tunandaa mashamba wakati mvua zimeanza jambo ambalo linatupelekea kulima tukiwa tumechelewa na mvua kukatika kabla mazao yetu hayajakomaa ikumbkwe kuwa mvua hizi ni za msimu sio za muda wote hivyo basi ni vyema kutambua majira ya mvua hizi kwa ajili ya maandalizi ya kilimo.
2. kilimo cha kisasa kinahitaji shamba liwe na rutuba ya kutosha kwa ajili ya kupata mazao mengi. mara nyingi tumekuwa tukilima tu shamba miaka nenda rudi bila hata kujali je rutuba ya shamba hili bado ni nzuri kwa ajilli ya kimo cha zao unalolima hivyo basi moja ya maandalizi ya shamba mojawapo ya kuhakikisha ni kwamba shamba unaloliandaa lina rutuba ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha mazao kama halina unaweza kiliongeazea kwa kuweka mbolea ya asili au mbolea inayouzwa madukani
3. kupanda begu bora ambazo zitaota vizuri na kutupelekea kuvuna mazo mengi. bengu bora ni zile zinazopatikana madukani na si kwingineneko mara nyingi tumekuwa tukipanda mbegu ambazo tunakua tumetunza au kunua zile ambazo zimepelekwa sokoni aidha kwa ajili ya chakula mbegu hizi sio bora kitaalam maana sio zote zinazoota ukipanda kwa hiyo hupelekea kuacha nafasi wazi sehemu ya shamba ambayo wakati mwingine inatulazimu kurudia kupanda upya.
4. kupanda kwa kufuata utaalamu wa upandaji ni, ni vyema ukamshirikisha mtaalamu wa kilimo hasa maafisa wa kilimo kwa ajili ya kukuelekeza namna ya ubandaji ambao utakuwezesha kupata mazao bora.
Hizo ndizo moja ya tofauti za kilimo cha kisasa na kilimo cha zamani na nyinginezo nyingi. Baada ya kujiakikishia kilimo bora na mavuno ya kutosha inatupaswa kutumia vyema mavuno tuliopata ili kuendelea kujiimarisha kuichumi na kimaendeleo zaidi.
Tuanayatumiaje mavuno yetu vyema ili tuweze tuweze kujiimarisha kiuchumi?
1. ni kuhakikisha tunapata soko la uhakika la mazao yetu, soko ambalo lina maslai makubwa kwetu sisi wakulima na sio wafanya biashara au wanunuzi wa mazao yetu,wote tunatakiwa kunufaiki kila mmoja kwa nafasi yake kwa namna hiyo basi inapaswa tushirikiane na serikali yetu katika kuuza mazao yetu kwani yenyewe ndiyo itakayo tusaidia kuuza mazao yetu bila ya kunyanyaswa.
2. baada ya kuuza mazao yetu tutumie vyeama pesa tuliopata. Kila mmoja awe na malengo juu pesa aliyopata, na moja ya malengo ambayo kila mmoja atayaweka katika akili yake juu ya pesa anayopata kutokana na kilimo ni kama ifuatavyo kujenga nymba bora, kuhakikisha watoto wanakwenda shule na kupata elimu bora kubuni miradi mbalimbali ambayo itamhakikishia kipato hata bila ya kulima.
Haya ndiyo yalikuwa malengo ya Godfrey chacha wakati anabuni huo mpango wa GODFREY FREEDOMAN’S FUND nikilenga kujikomboa na kuwakombo vijana wenzangu hasa wa jamii hii ya mkoa wa Mara lakini nikaona Dunia sasa imekuwa kijiji kwa nini mpango huu nisiwashirikishe vijana wote wa kitanzania ambao naamini adha yetu ni moja? kwa kufanya hivyo nikaleta swala hili kwenu Watanzania wenzangu tena wachapa kazi tuachane na dhana ya kusema kwa sisi ni masikini kwa sababu Taifa letu ni masikini mimi nasema sisi si masikini na Taifa letu si masikini ila tu tushiriki kufanya kazi na viongozi wetu pia washiriki vyema kusimamia kazi zetu na kutupa sapoti pindi tunapohitaji msaada wao aidha wa kimawazo, uwezeshaji na mabo mengine mengi.
tumeona hapo juu nimejaribu kungumzia ni namna gani jamii wa watu wa msoma wanaweza kujikwamua kotokana na umasikini wao kwa njia kilimo kulingana na mazingira yao je wewe kijana unaeishi mjini na huna sehemu ya kulima utafanyaje? je ufunge safari uende kijijini kukalime? au uendelee kutafuta maeneo ya wazi yalioko mjini ukalime hapana majibu ya maswali haya tutayapata kitika somo lijalo cha msingi ni kukaa makini na kuendelea kunifuatilia katika ukurasa wangu wa facebook kwa kutafuta GODFREY FREEDOMAN’S FUND au kutembelea blog yangu ya www.kisumwavillagematukio.blogspot.com au E-Mail: godfreychacha45@gmail.com au piga simu No. 0753 450 283 /0688 140 350.